Askofu na Mwimbaji mkongwe wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Ephraim Mwasasu amefariki Dunia mapema leo hii.
Taarifa za awali zinasema Mchungaji Ephraimu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Moyo.
Askofu Ephraim Mwasasu alikuwa ni kiongozi wa Makanisa ya Hossana Assemblies of God, Dar es salaam, Tanzania.
Gospo Media inaungana na Kanisa pamoja na familia ya Mchungaji Ephraim Mwasasu kwa kuomba na kuomboleza katika msiba huu mkubwa.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe.
Source: GospoMedia.