GOSPOTIMES

TOFAUTI KATI YA MLEZI (MENTOR) NA MTU WA MFANO WA KUIGWA (ROLE MODEL). – Dr. Zakayo Nzogere

✨ I. MAANA YA MALEZI (MENTORSHIP):

Malezi (Mentorship) ni mahusiano kati ya watu wawili ambapo mmoja anakuwa na uzoefu, ufahamu, na mtandao mpana zaidi katika jambo au nyanja husika. Katika mahusiano hayo, Mlezi (Mentor) anakuwa tayari kumsaidia “Anayelelewa” (Mentee) kufika kiwango alichopo Mlezi (Mentor) au hata zaidi yake.

📌 Malezi (Mentorship) ni mchakato ambao mara zote unahitaji pawepo na UHUSIANO na MAWASILIANO ya karibu kati ya Mlezi (Mentor) na Mlelewa (Mentee).

📌 Mlezi (Mentor) ni mtu anayechukua muda kukufahamu kibinafsi na kujua aina ya changamoto unazopitia.

MAMBO MUHIMU KATIKA ULEZI AU KULELEWA (MENTORSHIP):

 1. Mentor lazima awe na uzoefu au maarifa zaidi katika jambo husika.
 2. Lazima pawe na mahusiano binafsi.
 3. Lazima pawe na mawasiliano binafsi.
 4. Lazima Mlezi (Mentor) akubali kutoa muda wake, uzoefu wake, na hata mali zake ili kumsaidia “Mlelewa” (Mentee).
 5. Mentor ni mtu unayeweza kuwasiliana nae na kupata majibu na maelekezo toka kwake moja kwa moja (directly).

✨ II. MTU WA MFANO WA KUIGWA (ROLE MODEL):

📌 Ni mtu yeyote anayeangaliwa au kufuatwa na wengine kama kielelezo.

📌 Ni mtu ambaye tabia yake, juhudi yake, na mafanikio yake yanawatia wengine hamasa.

📌 Role Model ni mtu ambaye kazi yake inazungumza hata baada ya yeye kuondoka duniani.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIWA KWA MTU WA KUIGWA (ROLE MODEL):

 1. Awe na sifa njema.
 2. Awe na mafanikio unayotamani kuyafikia au kuzidi alipofika yeye.
 3. Siyo lazima uwe na mahusiano au mawasiliano binafsi; unaweza kumfanya mtu kuwa ROLE MODEL wako hata kama hamfahamiani wala yeye mwenyewe hajui kwamba unamuiga.
 4. Unaweza kujifunza toka kwa “Role Model” wako kwa kupitia vitabu vyake, makala, vipindi redioni, TV, Mtandaoni, kuhudhuria semina zake au makongamano, na kwa kusikiliza historia yake toka kwa wengine.
 5. “Role Model” anaweza kuwa mtu ambaye tayari amekufa siku nyingi lakini kazi na historia yake bado inazungumza na kukutia moyo katika jambo unalolifanya.

✅ ZINGATIA HAYA:

 1. HUWEZI KUMUITA MTU MLEZI (MENTOR) KAMA HAUNA “MAHUSIANO” NA “MAWASILIANO” BINAFSI (USO KWA USO, KWA SIMU, BARUA/BARUA PEPE, NK). HAIWEZEKANI KUWA NA MENTOR WA KWENYE TV AU YOUTUBE TU‼️
  ILI MTU AWE “MENTOR” WAKO NI LAZIMA YEYE AJUE NA AKUBALI KUFANYA JUKUMU HILO (Mentor/Mentee Relationship).
 2. UNAWEZA KUMUITA MTU “ROLE MODEL” WAKO HATA KAMA HAMJAWAHI KUONANA, KUJUANA, AU KUWASILIANA; ILI MRADI MAISHA YAKE AU KAZI ZAKE ZINACHOCHEA HAMASA NDANI YAKO YA KUINUKA AU KUFANIKIWA ZAIDI.
 3. UNAWEZA KUWA NA “ROLE MODEL” HATA AMBAYE NI MAREHEMU AU ALIYEISHI KARNE NYINGI ZILIZOPITA.

✅ WAKATI MWINGINE, MTU MMOJA ANAWEZA KUWA “MENTOR” NA WAKATI HUOHUO AKAWA “ROLE MODEL” WAKO KWA KUZINGATIA VIGEZO NA MASHARTI HUSIKA.

NB:
Wengi huwa tunachanganya matumizi ya neno “MENTOR” na “ROLE MODEL”.

Hata hivyo ninaheshimu tafsiri na ufahamu wa wengine katika jambo hili. Asante!!
(Dr. Zakayo Nzogere).

Leave a Comment