Prophet TB Joshua wa kanisa la Synagogue Church of all Nation (SCOAN) nchini Nigeria amefariki dunia.

Taarifa ya kifo cha Nabii TB Joshua zilianza Kama uvumi lakini muda mfupi uliopita taarifa maalum iliyotolewa kwenye kurasa rasmi za mitandao yake imethibitisha kifo chake bila kutaja sababu iliyopeleka kifo chake.
Taarifa hiyo imesema kuwa Siku ya Jumamosi Nabii TB Joshua ambaye tarehe 12 Mwezi huu angekuwa anatimiza Miaka 58 , alizungumza na wadau wa Emmanuel TV inayomilikiwa na kanisa hilo na kuwapa ujumbe kuwa katika kila Jambo Kuna majira yake huku ujumbe wake wa mwisho ukiwa ni “Kaeni Macho mkiomba”.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe.
Mwandishi: Deborah Mwita